Na Mwandishi wetu, Arusha
Naibu
Waziri wa Afya Dr Faustine Ndungulile amewataka wanamuziki wa Injili
kuimba nyimbo zinazoweza kuihamasisha jamii kushiriki katika masuala
mbalimbali ikiwamo uchangiaji wa damu salama.
Akizungumza
wakati wa Tamasha la Tamani Festival lililoandaliwa na Mtandao wa
Wasanii wa Tansia ya Injili (Tagoane) Dk Ndungulile alisema yapo mambo
mengi yanayohitaji ushiriki wa wasanii katika kukabiliana nayo.
"
Yapo matukio yanawategemea wasanii mshiriki, imbeni nyimbo
zinazoihamasisha jamii ipime magonjwa, iache uovu maana matukio ya
kikatili nayo," alisema.
Dr
Ndungulile ambaye ni muasisi wa uchangiaji wa damu nchini alisema uhai
wa mama na mtoto pia unategemea uhakika wa damu salama.
Pia
alikubali ombi la kuwa mlezi wa Tagoane akiahidi kushirikiana na
wanamuziki kuhamasisha jamii kupima afya zao hasa wanaume ambao wengi
hawashiriki.
Awali Rais
wa Tagoane Dr Godwin Maimu alisema taasisi hiyo imeamua kufanya tamasha
la asante mama ili kuenzi mchango wa mwanamke katika jamii.
Pamoja
na mambo mengine Tagoane walishiriki kufanya usafi katika hospitali ya
Mount Meru na kuhamasisha uchangiaji wa damu salama.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dr
Faustine Ndungulile na Rais wa Tagoane wakutandika moja ya mashuka
yaliyotolewa na Tagoane katika Hospitali ya Mount Meru Mkoani Arusha
DR.NDUGULILE: “WASANII IMBENI NYIMBO ZINAZOIHAMASISHA JAMII IACHE UOVU"
Reviewed by Erasto Paul
on
July 01, 2018
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili