Na Mwandishi wetu, Arusha
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema Serikali itaendelea kuunga mkono
jitihada za vyama vya wasanii vinavyojikita katika mbalimbali zinazoleta
maendeleo ya Taifa.
Shonza amesema hayo baada ya
kushuhudia kazi zinazofanywa na Mtandao wa Tasnia ya Wasanii wa Muziki wa
Injili Tanzania (TAGOANE) ikiwamo ya kuhamasisha jamii kuchangia damu salama
ili kuokoa uhai wa mama na mtoto kupitia tamasha la Mama ni wa Thamani ( TAMANI
FESTIVAL).
Akizungumza katika tamasha hilo
jijini Arusha, Shonza alisema kazi ya sanaa sio tu kutoa burudani peke yake
bali kuisadia jamii kuondokana na changamoto mbali mbali zinazowakabili.
" Tagoane ni kati ya taasisi
makini za wasanii iliyoonyesha njia kwamba kumbe inawezekana kutumia burudani
kuhamasisha jamii kuondokana na changamoto, ni wakati wa taasisi nyingine kuiga
mfano huu," alisema.
Shonza alisema Serikali ipo tayari
kufanya kazi na kuunga mkono vikundi vya wasanii vinavyoweza kutumia sanaa yake
kuleta matokeo chanya kwa taifa.
Alisema tamasha la mama ni wa
thamani linamuongezea heshima mwanamke wa kitanzania kwa kuwa ni ukweli
usiopingika kuwa anao mchango mkubwa katika jamii yake.
Awali Rais wa Tagoane, Dk Godwin
Maimu alisema wasanii wa injili waliamua kuandaa tamadha hilo kuenzi mchango wa
wanawake wa kitanzania katika kupigania maendeleo ya taifa lao.
" Sekta ya afya inatuambia
upungufu wa damu ni kati ya sababu za vifo vya wanawake wakati wa kujifungua,
sasa katika kuitambua thamani ya mwanamke tumefungua kampeni ya kuchangia damu salama
kuokoa uhai wa mama na mtoto," alisema.
Alisema kampeni hiyo itafanyika pia
katika mikoa ya Manyara, Mbeya, Dar es Salaam na Dodoma na lengo kubwa ni
kuihamasisha jamii kuvhangia damu salama.
Mbali na shughuli nyingine, TAGOANE
walifanya usafi na kutoa msaada wa mashuka zaidi ya 400 kwa hospitali ya Mount
Meru mkoani Arusha.
Baadhi ya wanamuziki wa muziki huo
wa Injili walisema jukumu lao kubwa ni kuhakikisha wanahubiri neno la Mungu kwa
njia ya uimbaji pamoja na kufanyia kazi kwa vitendo yale wanayoyaimba.
SHONZA: “SERIKALI ITAENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA VYAMA VYA WASANII”
Reviewed by Erasto Paul
on
July 02, 2018
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili