TAGOANE WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUHAMASISHA UCHANGIAJI DAMU ARUSHA.

Na mwandishi wetu, Arusha

Mji wa Arusha leo ulizizima baada ya wadau wa Mtandao wa Wasanii wa Injili Tanzania Kwa kiingereza Tanzania Gospel Artists Network – kufanya maandamano ya amani kuhamasisha jaamii kuchangia damu ili kuokoa uhai wa mama na mtoto.

Tagoane walifanya maandamano hayo wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiruthel Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Arusha Mashariki, Dk Solomoni Masangwa baada ya kufanya usafi na kutoa zawadi katika Hospitali ya Mount Meru kupitia tamasha la Asante mama linaloitwa TAMANI Festival.
Mwimbaji wa Jimbo la Injili Tanzania na Mwanahabari wa Gazeti la Mwananchi Dokta.Tumaini Msowoya Akifanya Usafi Nje ya Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mount Meru Arusha.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Tagoane Dk Godwin Maimu alisema wameamua kufanya maadhimusho hayo ili kutambua mchango wa mama katika malezi ya familia, jamii na taifa.

" Tumeanza tamasha hili leo ya kufanya usafi, kutoa zawadi hospitali na kufanya maandamano ili tuitumue jamii yetu ujumbe kwamba mama ni wa thamani," alisema.

Shughuli zote za uchagiaji wa damu zinaendelea kufanywa katika viwanja vya Shekh Amri Abeid Karume..

Kwa upande wake Askofu Dr Masangwa alisema jamii haina budi kuunga mkono harakati za kumuenzi mama kwa kuwa ni mtu wa muhimu kwa kumu hakikushia ulinzi na kuepuka vitendo vya kikatili dhidi yake.

Tagoane wanaendelea kufanya tamashavhilo la siku tatu ambalo Naibu Waziri wa Afya, Dr Faustine Ndungulile atazindua uchangiaji wa damu na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Juluana Shonza atazindua tamasha siku ya jumapili.

Mwisho.
TAGOANE WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUHAMASISHA UCHANGIAJI DAMU ARUSHA. TAGOANE WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUHAMASISHA UCHANGIAJI DAMU ARUSHA. Reviewed by Erasto Paul on June 29, 2018 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.