Watu watano wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wameuawa katika eneo la Toangoma jijini Dar es Salaam, katika majibizano ya risasi na Polisi yaliyotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lukula amesema walipata taarifa
kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna njama za uhalifu zimepangwa kufanyika
maeneo hayo usiku wa jana, hivyo wakajipanga kwa ajili ya kudhibiti.
Amesema
ilipofika muda walioambiwa kweli wahalifu hao ambao idadi yao haikuweza
kupatikana, lakini walikuwa wengi, wakafika eneo la tukio na kupambana na
polisi.
“Majibizano
ya silaha yalikuwa makubwa kwa sababu walikuwa na silaha nzito, lakini Jeshi la
Polisi lilijipanga imara kuwadhibiti na kufanikiwa kuua watano na wengine
wakatokomea kusikojulikana,” amesema.
Amesema
wananchi wasiwe na hofu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili
kunusuru usalama wao na mali zao.
“Tumejipanga
na tunapopata taarifa za uhalifu, pamoja na askari wetu kuwa doria maeneo hayo,
lakini hujipanga upya kwa ajili ya kupambana na tukio husika.”
Watano wafa katika majibizano ya risasi na polisi Temeke.
Reviewed by Erasto Paul
on
October 06, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili