Dar es
Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehoji maswali kibao
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Inspekta Jenerali wa
Polisi(IGP), Simon Sirro kuhusu mambo yanayoendelea kwenye upelelezi wa Ben
Saanane, Tundu Lissu na aliyemtishia Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
Saanane ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
ambaye hajulikani aliko na Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki ambaye alipigwa
risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu.
Katika
mkutano na waandishi wa habari leo Ijumaa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na
Mambo ya Nje wa Chadema ameanza kwa kusema, “Ni siku 695 tangu
Mawazo(Alphonce) auawe, siku 326 tangu Ben Saanane apotezwe na watu
wasiojulikana na leo ni siku 26 tangu Lissu afanyiwe jaribio la kumuua na mpaka
sasa polisi hawajasema lolote, zaidi ya Nissan 8 na zimehifadhiwa
kusikojulikana,”
“Leo
tunapozungumza, viongozi mbalimbali wanaendelea kutishwa, Mbunge wa Bunda,
Ester Bulaya anatishwa na watu wamemfuata nyumbani kwake, Josua Nassari
ametishwa, Lema(Godbless) ametishwa,”
“Ben
Saanane alitishwa na alitoa taarifa Kituo cha Polisi Tabata na kapotea, Lissu
alitoa taarifa kwamba anatafutwa na yaliyotokea mnajua,”
“Hofu ni
kubwa, maiti zaidi ya 17 zimeokotwa Coco Beach hakuna ‘seriousness’ kwa
matukio,” amesema Mrema
“Waziri
anatishwa mbele ya kamera na hakuna jitihada, IGP anasema hajui alipo, hii
inaonyesha hakuna ‘seriousness’ katika kupambana,” amesema Mrema
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Kigaila Benson amesema,
“Haya mambo si ya kawaida, yanafanywa na watu wasio wa kawaida, niseme tu
hakuna aliye salama, hujui kesho yako,”
“Kuna
kijana anaandika mambo ya ajabu, kwa nini polisi hawaoni, IGP anachagua mambo
ya kusikia, kwa nini ukimkosoa Rais jioni yake unakamatwa,”
“Kama
polisi wanaona, hawachukui hatua? Walipouawa polisi pale Mbagala, watu
waliotuma picha walikuwa Mahenge, walikamatwa sasa huyu kijana anafanya nini?
“Wanasema
wamekamata Nissan, hivi hizi Nissan zilikuwa wapi, zilikuwa zinaendeshwa na
nani? Hii si ni kanya boya?
“Waziri
Mwigulu anasema gari alilolitaja Lissu liko Arusha, waziri ametumia kigezo au
kifaa gani kubaini gari halikuwahi kufika Dar? Kwa nini chombo hicho kisitumike
kuwabaini waliomshambulia Lissu?
“Mwigulu
kwa nini amechukua uwakili wa mtuhumiwa? Amehojiana vipi na huyo? Kwa nini mtu
huyo anayetuhumiwa asikamatwe na sasa anafanya kazi ya kumtetea?
“Polisi
wanatakiwa kutuambia, upo wapi usalama wa Rais,” “Tumesimama upepelezi wa tukio
la Lissu kwa sababu ya dereva, ina maana kama dereva angekufa upepelezi usingekuwapo?
“Sisi
hatuwezi kumficha dereva, anapata matibabu, ila kama wamesema
wanafahamu gari lile lipo Arusha wanashindwaje kwenda kuzungumza na dereva,”
amehoji Kigaila
“Sirro
analitumia jeshi kisiasa, Sirro kwa nini asimuulize RPC Kaganda(Suzan)
aliyekuwa Kinondoni ambaye alikuwapo siku Nape anatolewa bastola kwa nini
hawakumkamata,”
“Jeshi la
polisi ni letu sote, tusilitumie kisiasa, tunataka tueleweke kwamba IGP
wanamjua huyu mtu,”
“Kwa nini
wanamtafuta mtu ambaye walikuwa naye, hivi kwa nini maswali magumu wanakuwa na
majibu ila maswali mepesi wanakosa majibu,”
Chadema wahoji maswali kibao sakata la Lissu, Saanane, aliyemtisha Nape
Reviewed by Erasto Paul
on
October 06, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili