Wakati wanawake wengi weusi wakijitahidi kubadilisha ngozi zao kuwa weupe kwa gharama yoyote ile hii inakuwa tofauti kabisa na mawazo ya Mwanamitindo (Model) Martina Big kutoka Ujerumani
Martina Big
Martina (28) amesema alitumia dola $50,000 sawa na Tsh milioni 112 kwa kufanya upasuaji mdogo wa matiti na kubadili ngozi yake kabisa.
Martina Big kabla ya kubadilisha muonekano
“Nilijiona mimi ndiye nilikuwa mwanamke mwenye matiti makubwa barani Ulaya ndipo nikaamua kuongeza ukubwa wa matiti na nimefanikiwa naamini naonekana kama wao ,”asema Martina.
Akiingia kwenye studio za ITV
“Sipendi kabisa kukwazana na watu weusi na navutiwa na rangi zao nilikuwa nikiota kuwa kama wao na ndoto yangu imetimia, Najiona ni mwanamke mweusi na ndio maana nimepanga kuwa januari mwakani nitaenda Afrika kujifunza tamaduni za huko,“amesema Martina.
Martina alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo kufananishwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi, amesema watu wengi wamekuwa wakimfikiria hivyo ila yeye hana lengo hilo na hajawahi kufikiria kuhusu ubaguzi wa rangi.
Martina amesema msukumo wa kubadilisha rangi yake umekuja baada ya kuvutiwa na muonekano wa Pamela Anderson na Katie Price.
“Nataka nionekane kama mtoto ila niwe na matiti makubwa, kama Pamela au Katie mara ya mwisho nilipo onana nao nilikuwa mweusi na mwenye nywele nyepesi lakini kwa sasa nimekuwa mweusi na nywele ngumu najivunia,”amesema Martina.
Hata hivyo mrembo huyo amedai kuwa kabla ya mwezi januari mwakani atafanya operation ndogo ya pua ili iendane na muonekano wa kiafrika na tayari rafiki yake wa kiume ameshamruhusu kufanya hivyo.
Martina Big na Boyfriend wake.
Mwanamke huyo amesema kwa sasa tayari mwili wake umeanza kukataa baadhi ya vyakula vya kizungu na ameanza kupenda muziki kutoka Afrika na Marekani.
Model wa kizungu atumia mil. 121 kubadilisha rangi kuwa mweusi.
Reviewed by Erasto Paul
on
October 05, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili