Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro
amefunguka na kuwataka wanasiasa nchini kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi
ikiwepo upelelezi wa tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu
Lissu.
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Godbless Lema wa Arusha pamoja na Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini ni kati ya wabunge ambao walionyesha kusikitishwa na kauli ambayo aliitoa IGP Sirro akiwa mkoani Mtwara kuhusu uchunguzi wa sakata la Tundu Lissu na kusema kuwa dereva wa Lissu anachelewesha upelelezi wa sakata hilo.
Wabunge hao walikwenda mbali zaidi na kusema wao wanaona jeshi la polisi halihitaji kufanya uchunguzi wa kina juu ya sakata hilo kwa kuwa jeshi hilo linafahamu nini kipo nyuma ya tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma. Kufuatia kauli hizo IGP ndipo amefunguka na kuwataka wanasiasa kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwa pamoja na uchunguzi wa sakati hilo.
Kamanda sirro amesema kauli
za wabunge na wanasiasa wengine kuhusu uchunguzi juu ya tukio hilo zinaonekana
kutaka kuingilia majukumu ya Jeshi la polisi kwani wao wanajua wajibu
wao.
Aidha amesema kwa kuwa wao
ni wanasiasa wanapaswa kuendelea kuongea kwa kuwa Kuongea ni kazi yao.
Pamoja na mambo mengine pia
amelitaka jeshi la polisi mkoani hapa kutumia vyombo Mbalimbali vya
habari kuwaelimisha wananchi juu ya mauaji yanayotokana na imani za Kishirikina
kwani njia pekee ya kukomesha tatizo hilo ni kwa kutoa elimu.
Mkoa wa njombe umekuwa ukikumbwa
na mauaji mbalimbali yanayohusishwa na imani za kishirikina pamoja na kulipiza
visasi.
IGP Sirro awaonya wanasiasa Juu ya Sakata la Tundu Lisu
Reviewed by Erasto Paul
on
October 06, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili