Dar es
Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru mfanyabiashara Yusuph
Manji(41) baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha shtaka dhidi yake.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za
kulevya iliyokuwa ikimakabili Manji.
Hukumu
hiyo imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian
Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.
Katika
kesi hiyo, upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi saba na wa mashtaka kuwa na mashahidi watatu.
Awali,
Manji kupitia wakili wake Hajra Mungula aliieleza Mahakama kwamba angekuwa na
mashahidi 15.
Katika kesi
hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani
Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Ushahidi
wa upande wa utetezi mahakamani unaonyesha Manji ana vyuma kwenye moyo.
Mfanyabiashara
huyo katika utetezi wake alidai ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka
kwa babu zake na alianza kuugua akiwa na miaka 26.
Mahakama yamuachia huru Manji
Reviewed by Erasto Paul
on
October 06, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili