Wageni wengine wa heshima kwenye uzinduzi huo
ni Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini,
Mchungaji Peter Msigwa, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah, Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha Baby Baraka Chuma, wachungaji kutoka
makanisa mbalimbali.
Akizungumza na Mwanaspoti, Msowoya alisema
tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.
“Naenda Iringa kurudisha shukrani zangu kwao,
nataka wajue nipo huku sio tu kwa sababu ya kazi bali huduma ya kuimba
niliyoanza ”
Alizitaja nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa
ni Hakuna Matata, Mwamba, Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu, Wanawake Jeshi
Kubwa, Samehe na Mungu wa Rehema.
“Kazi hii nimeifanya chini ya usimamizi wa JB
Production ikisimamiwa na Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye meneja
anayesimamia kazi zangu kwa sasa,’ alisema Msowoya.
Wasanii
watakaomsindikiza
Meneja wa Msowoya, Smart Bilionea Producer
Baraka alisema tayari waimbaji na kwaya mbalimbali kutoka Iringa na Dar es Salaam
watamsindikiza kwenye uzinduzi huo.
Alizitaja kwaya zizothibitisha kumsindikiza kuwa
ni Wakorinto wa Pili kutoka Mufindi, Muhimidini na kwaya ya Vijana kutoka
Iringa mjini.
Baadhi ya waimbaji ni Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu
ni Mungu tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine maarufu
kwa jina la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses Simkoko, Ritha Komba
na Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.
Wengine ni Rebecca Baraka, Jesca Msigwa, Ester
Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis Lukosi, Wadi Mbelwa, Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu
Mgogo, Emma Sanga na Victoria Mwenda kutoka Iringa.
“Waimbaji watakaomsindikiza ni wengi nab ado tunaendelea
kuwasajili wengine. Bado tupo kwenye mazungumzo na Bahati Bukiku ambaye
anaangalia ratiba yake, ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.
Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya kutokana
na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.
Historia
Hakuna Matata ni albamu ya pili ya Msowoya baada
ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.
“Bahati mbaya niliitengeneza kutokana na kiwango
kidogo hivyo iliishia kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii ni nzuri
na wakazi wa Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.
Hakuna Matata’ ya Tumaini Msowoya kuachiwa albamu yake October 29 Iringa mjini
Reviewed by Erasto Paul
on
October 18, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili