Moto waacha Vilio Makete, Shule yaponea Chupuchupu


Moto Mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana umezuka na kuunguza Mali za wananchi katika kata ya Mbalatse wilayani Makete mkoani Njombe

Moto huo uliozuka tangu Jana umeunguza nyumba zaidi ya 5 pamoja na mashamba ya Miti ya wananchi

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessy amefika kujionea madhara hayo akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa halmashauri Mh Egnatio Mtawa kaimu Mkurugenzi Mtendaji Gregory Emannuel na maafisa wengine wa serikali
Shule ya sekondari Mbalatse ni miongoni mwa taasisi iliyonusurika kuteketea kwa moto huo licha ya mashamba yake ya miti kuungua na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu wao walishiriki kuudhibiti moto huo

Hadi tunaondoka eneo la tukio saa 12 jioni moto huo ulikuwa bado haujazimwa wote na juhudi zilikuwa zinaendelea
 Msitu wa shule ya sekondari Mbalatse ukiteketea kwa moto
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy (mwenye blauzi nyekundu) akikagua madhara ya moto huo hii leo



 Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbalatse wakihamisha vifaa vyao visiungue moto



 Bibi ambaye nyumba yake imetekekea kwa moto akisononeka
 Vilivyonusurika kwenye nyumba ya bibi huyo
 Nyumba ya bibi huyo ikiungua






Moto waacha Vilio Makete, Shule yaponea Chupuchupu Moto waacha Vilio Makete, Shule yaponea Chupuchupu Reviewed by Erasto Paul on October 19, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.