DC Ludewa awaagiza Walimu kutoa Adhabu kali kwa wanafunzi wakorofi.


Mkuu wa wilaya ya Ludewa mh. Andrea Tsere akizungumza na viongozi pamoja na wazazi katika shule ya sekondari St. Alois Ludewa,


Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne 2017 shule ya wasichana St.Alois Sekondari Ludewa

Mkuu wa wilaya ya Ludewa mh. Andrea Tsere akizungumza na viongozi pamoja na wazazi katika shule ya sekondari St. Alois Ludewa,

Ni picha ya pamoja Dr.susan Kolimba, Dc Ludewa na viongozi wengine pamoja na wanafunzi
 Na Maiko Luoga Ludewa. 
 Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Mh. Andrea Tsere amewaagiza walimu wakuu wa shule za Msingi na sekondari wilayani humo kuhakikisha wanatoa adhabu kali kwa wanafunzi ambao hawafuati maagizo ya walimu darasani kwani wanafunzi wakorofi ndio chanzo cha wilaya ya Ludewa kufanya vibaya kitaaluma na kutoa onyo kali Kwa Wazazi wanaowalalamikia walimu bila sababu za msingi. 

Aidha amewataka walimu wanaoshindwa kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule zao kwa darasa la saba na kidato cha nne kila mwaka kujitathmini na kuacha kazi maramoja wilayani Ludewa kwakuwa walimu wanaotafuta kazi wako wengi mitaani na wamekuwa na uwezo mkubwa kuliko walimu ambao wapo kwenye ajira na wamekuwa wakishindwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye shule zao. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Tsere alitoa maagizo hayo kwa msisitizo mkali mbele ya naibu waziri wa Mambo ya nje ya nchi na ushirikiano wa Africa mashariki kikanda Dr. Susan Kolimba alipokuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya Tano Katika shule ya sekondari ya wasichana St. Alois Ludewa mjini iliyofanyika tarehe 14 mwezi huu October 2017.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Ludewa aliwaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuwafuatilia na kuwapima mimba kila mwezi wanafunzi hao wakike kwakuwa baadhi yao wamekuwa wakijihusisha na masuala ya mapenzi na vijana wa mitaani na wengine ni watumishi wa serikali nakuongeza kuwa mwanaume yeyote atakayekutwa amesimama au anajihusisha na mapenzi na wanafunzi hukumu yake ni kifungo cha miaka 30 jela bila msamaha. 

Kwaupande wake naibu waziri wa Mambo ya nje ya nchi na ushirikiano wa Africa mashariki kikanda Dr. Susan Kolimba amewataka wahitimu watakao fanya mtihani wao wakuhitimu kidato cha nne October 30 mwaka huu kutulia na kufanya vizuri mitihani yao ili baada ya hapo waweze kupata matokeo mazuri hasa Division One na two hatimae waendelee na masomo ya elimu ya juu.
DC Ludewa awaagiza Walimu kutoa Adhabu kali kwa wanafunzi wakorofi. DC Ludewa awaagiza Walimu kutoa Adhabu kali kwa wanafunzi wakorofi. Reviewed by Erasto Paul on October 16, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.