TUNDU LISSU;- I survived to tell the tale,Please keep up the fight"

http://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/09/Tundu-Lisu.jpg
Usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi nchini Kenya anadaiwa kufungua kinywa kwa mara ya kwanza.

Lissu anadaiwa kumpa ujumbe Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kwamba amenusurika kifo ili aje auanike mkasa mzima.

Kwa mujibu wa taarifa ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, imedai Lissu alizungumza na Mbowe usiku wa jana kwa mara ya kwanza.

"Mwenyekiti I survived to tell the tale. Please keep up the fight" ni maneno machache aliyosema Lissu jioni hii baada ya kufumbua kinywa! ameandika Lema.

Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake, nyumbani kwake mjini Dodoma muda mfupi baada ya kutoka bungeni.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kati ya risasi zaidi ya 30 zilizoelekezwa kwa mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), risasi tano zilimpata mkononi, mguuni na tumboni.
TUNDU LISSU;- I survived to tell the tale,Please keep up the fight" TUNDU LISSU;- I survived to tell the tale,Please keep up the fight" Reviewed by Erasto Paul on September 11, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.