Mtuhumiwa wa Utekaji, Samson Peter
Mtuhumiwa wa utekaji wa watoto
Arusha, Samson Peter amefariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu
kuwakimbia Polisi alipokuwa amekwenda kuwaonyesha washirika wenzake wa utekaji
eneo la Muriet Mkoni Arusha.
Akithibitisha kutokea kwa kifo chake Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa mtuhumiwa huyo wa utekaji
alipigwa risasi ya mguuni kama onyo la kujaribu kumtoroka Askari aliyekuwa
ameongozana naye majira hayo ya saa 5:30 usiku.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa baada ya tukio hilo
la kumjeruhi mtuhumiwa Samson Peter kwa nia ya kumuadhibu alifikishwa
Hospital ya Mt. Meru lakini alifariki kutokana na kuvuja damu nyingi kwenye
jeraha la mguu.
"Ni kweli mtuhumiwa amefariki.
Ambapo jana usiku wakati alipokuwa amesindikizwa na polisi kuwaonyesha
waashirika wenzake alitaka kutoroka, lakini katika hatua ya kumuadhibu kwa
kitendo chake hicho ndipo akapigwa risasi ya mguuni ambapo ilimpelekea kuvuja damu
nyingi na alifariki baada ya kufikishwa hospitali" Kamanda Mkumbo.
Aliyeteka watoto Arusha auawa na Polisi.
Reviewed by Erasto Paul
on
September 07, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili