UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE WAPUUZIA MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI.


Mamlaka Inayosimamia hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe- Kibena imepuuzia agizo lililotolewa na Naibu waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala ambalo liliwataka kuboresha Huduma ya Vyoo katika vyumba vya kujifungulia kwa akina mama wajawazito.

Dkt Kingwangala amebainisha hao alipofanya ziara ya kushtukiza katika katika Hospitali Hiyo ziara iliyolenga kukagua hali ya utolewaji wa huduma za afya pamoja na kujiridhisha utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mapema mwaka jana.

Achilia mbali Tatizo la Vyoo Pia amebaini uchakavu wa vitanda na Kukosekana kwa umakini katika usafi kwa mujibu wa kanuni za afya.

‘Ambacho naona hakipo sawa ni vitanda nafikiri mmeona wenyewe vitanda vingi vya zamani havijafanyiwa matengenezo,wala sio vya kutupwa,wao wanadhani hivi vitanda ni vya kutupwa wanatakiwa wavifanyie ukarabati ,nimewaagiza wavirekebishe ili viendane na hadhi ya hospitali yenyewe ya mkoa’’amesema Dkt Kingwangala.

‘Vyoo vyote katika vyumba vya kujifungulia havifanyi kazi,wanasema havifanyi kazi lakini kimsingi vinatumika hivyohivyo,mama akizidiwa anatumia hivyohivyo lakini vipo katika hali mbaya,hili ni eneo ambalo wanapaswa kurekebisha’’Ameongeza Dkt Kingwangala.

Mara baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali yakiwemo ya vyumba vya uzazi amesema katika ziara ya mwaka uliopita hali hospitali hiyo ilikuwa mbaya zaidi ikilinganishwa na hali ya sasa.
Hata Hivyo ameupongeza uongozi kwa kutekeleza baadhi ya maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya mwaka jana.

Hospitali teule ya mkoa wa Njombe inaendelea na ukarabati wa jengo la duka la dawa baada ya kukamilisha ukarabati wa jengo la Maabara.
UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE WAPUUZIA MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI.  UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE WAPUUZIA MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI. Reviewed by Erasto Paul on July 17, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.