Mkuu wa shule ya sekondari Njombe {NJOSS } Benard William
Ikiwa ni
siku tatu tangu kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita, Shule ya Sekondari
ya Njombe imelilalamikia Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) ikidai matokeo
hayo hayaendani na wastani wake wa ufaulu (GPA) wa masomo.
Hata
hivyo, Dk Joseph Mbowe, ambaye ni mkuu wa Idara ya Teknolojia, Habari na
Mawasiliano (Tehama) wa Necta, amekanusha madai hayo akisema matokeo hayana
tatizo lolote isipokuwa ufaulu wa masomo kwa GPA haujapishana sana.
Kwa mujibu
wa matokeo yaliyotangazwa na Necta Jumamosi mjini Zanzibar, shule 10
zilizofanya vibaya, Njombe imeshika nafasi ya nne kutoka mkiani. Orodha hiyo
inajumuisha shule za Chasasa iliyoko Pemba, Kiembesamaki (Unguja), Mwenyeheri
Anuarite (Dar es Salaam), Ben Bella (Unguja), Meta na Mlima Mbeya (Mbeya),
Njombe (Njombe), Al-Ihsan Girls (Unguja), St Vincent (Tabora) na Hagafilo
(Njombe).
Mkuu wa
Shule ya Sekondari ya Njombe, Bernard William alisema hawakubaliani na matokeo
hayo kwa sababu kuna baadhi ya shule wamezipita kwa kutoa daraja la kwanza,
nafasi ya masomo na ufaulu wa masomo kwa GPA.
Alisema
kulinganisha na matokeo ya shule nyingine ambazo wanaona wamezizidi kwa kiwango
cha ufaulu, wanashangazwa kuwa nafasi ya 442 kati ya shule 449 zilizofanya
mtihani wa taifa.
“Tunaomba
kitengo cha Tehama cha Necta wapitie upya kwa kuwa matokeo hayaendani na ufaulu
wa masomo kwa GPA,” alisema William.
Akizungumzia
suala hilo, Dk Mbowe alisema mwaka huu wameangalia vigezo mbalimbali, kama
wanafunzi kupata alama “A” katika viwango vyao vya ufaulu shuleni.
Hata
hivyo, Mbowe alisema: “Nimewasiliana na mkuu wa shule na suala lake Necta
tunalifanyia kazi. Lakini katika shule yake tumebaini kuna changamoto ya
mwanafunzi wa kiume kuandikwa katika jinsi ya kike na hilo ni kigezo kimojawapo
tulichokiangalia,” alisema Dk Mbowe.
Alisema
kosa hilo lilifanyika tangu matokeo ya kidato cha nne na mwanafunzi huyo
aliomba marekebisho yafanyike.
Hata
hivyo, alisema bado katika matokeo ya kidato cha sita jina lake limeendelea
kutokea kwenye orodha ya wanafunzi wa kike, akilenga kuonyesha jinsi shule hiyo
ilivyofanya uzembe kushughulikia tatizo hilo.
Njombe sekondari yalalama kushika mkia matokeo kidato cha sita
Reviewed by Erasto Paul
on
July 18, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili