Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umesema Taifa
linapitia kipindi kigumu cha kuminywa kwa haki za binadamu.
Akizungumza leo Jumapili, Julai 16,
Mratibu wa Kitaifa wa mtandao huo, Onesmo Olengurumwa amesema tangu
kuanza kwa mwaka huu kuna matukio makubwa 20 ambayo yanaminya haki za binadamu.
Amesema wakuu wa mikoa na wilaya
wanakamata watu na kuwaweka mahabusu bila ya makosa.
Olengurumwa amesema hivi sasa mtu
akitoa maoni anakamatwa na kufunguliwa mashtaka kitendo ambacho ni uonevu.
Amesema kufanya mikutano ambayo ni
haki ya kisiasa inakatazwa bila ya kutolewa sababu za msingi.
Mratibu huyo amesema mtandao
unaangalia namna ya kuchukua hatua za kisheria kuhusu uvunjaji wa haki za
binadamu unaofanywa na Serikali.
THRDC watoa tamko hali ya haki za binadamu nchini 0
Reviewed by Erasto Paul
on
July 16, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili