Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amesema anayo
orodha ndefu ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM.
Polepole
amesema hayo leo huku akibainisha kuwa orodha hiyo inahusisha wenyeviti,
madiwani na wabunge lakini siku nyingi tu alikuwa amewakatalia kuwapokea.
Hata hivyo
Polepole amesema kwamba kutokana na kutuhumiwa kuwanunua sasa anafanya kweli,
atawachukua mmoja mmoja.
Polepole
amesema amemua kuchukua uamuzi huo baada ya Chadema kuonyesha utovu wa nidhamu
kwa kudai kuwa madiwani wanaokihama chama hicho wamehongwa na CCM.
“Sasa
tutaanza kumchomoa mmoja baada ya mwingine na kwa kutekeleza hilo wiki hii
watampokea kiongozi mkubwa wa chama hicho,’’anasema Polepole.
Amebainisha
kuwa kama chama kinakuwa na viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi
chama hicho kitakuwa ni cha hovyo
"Madiwani wamesema wanamuunga mkono John Magufuli, wametoka wenyewe wameanza kusema CCM imewanunua, sasa kwa vile wameanza utovu wa nidhamu nitaanza kumtoa mmoja baada ya mwingine,’’anasema.
"Madiwani wamesema wanamuunga mkono John Magufuli, wametoka wenyewe wameanza kusema CCM imewanunua, sasa kwa vile wameanza utovu wa nidhamu nitaanza kumtoa mmoja baada ya mwingine,’’anasema.
Polepople
anaongeza kwamba: “Nilikua nakataa kuwapokea ila nina orodha kubwa wapo
wenyeviti, wabunge kibao kama vile watu wanaojisaliji kodi ya majengo
TRA," amesema.
"Unajua wanasema wanaisoma namba, nawahakikishia baada ya miaka mitano kwa spidi hii iliyoanza nayo CCM namba inayoonekana wakati huu itakuwa haisomeki kabisa, nitafanya shoo ndogo tu kuwachomoa viongozi hao sipendi kwenda kuwachukua wengi sababu nitaonekana kama nawahujumu vile na pia ili upinzani usikose watu angalau wa kuzungumza nao,"amesema

Polepole awakaribisha wanaokimbia upinzani
Reviewed by Erasto Paul
on
July 16, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili