Andiko la Naibu waziri Afya Dkt Khamisi Kingwangala Kuhusu Ziara yake Mkoani Njombe.

DAY 7: Mkoa wa Njombe. 
 https://scontent-mxp1-1.xx.fbcdn.net/v/t1.0-0/p320x320/20229128_1456500121093500_1646317211353005753_n.jpg?oh=07df8838f76f2b70b2db0b23b3914222&oe=59C5F6C1
Hapa ziara inaendelea Wilaya ya Njombe, Hospitali ya Makambako. Tunatoa maelekezo ya kuanza huduma za upasuaji kwenye chumba kipya cha upasuaji kufikia tarehe 1 Agosti. 

Pia warekebishe changamoto ndogo iliyokuwepo kwenye jengo hili. Dr. Kyungu Ernest (maarufu kama kyungu.com) anaji-commit 'kupiga kisu' cha kwanza yeye mwenyewe.

 Nimependa spirit yake. Pamoja na mapungufu hayo, yeye na wenzake wamefanya kazi nzuri, mbali na theatre hii, wamejenga pia wodi mpya, kubwa na nzuri kwa ajili ya wazazi. 

Tumewapongeza sana kwa jitihada hizi. Pia Mhe. Deo Sanga, Mb., maarufu kama Jah People amejitolea kutanua eneo la vyumba vya kuona wagonjwa wa nje (OPD); tumempongeza sana na kumtaka aendelee na moyo huo. Huu ni uongozi utakaokumbukwa na watu.

 Changamoto iliyokuwepo ni ya ramani ya jengo hususan eneo la mtiririko wa mtoa huduma (flow). Anaingilia wapi, anabadilishia nguo wapi, ananawa mikono wapi, anaingilia theatre tayari kwa upasuaji wapi, na akimaliza anatokea wapi! Flow hii isipozingatiwa inaweza kuwa chanzo sugu/cha kudumu cha maambukizi ndani ya theatre (nosocomial infections).

 Madaktari wanakuwa wanafanya operesheni lakini vidonda haviponi haraka na wakati mwingine mishono inafunguka (gapping). Badala ya operesheni kuwa tiba mujarab, inageuka kuwa chanzo cha changamoto mpya kwa mgonjwa kuanza kupambana na ugonjwa mpya wa maambukizi.
 https://scontent-mxp1-1.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/20046408_1456500247760154_1783646182646921976_n.jpg?oh=1bdca831a4279691768f8c6c6e976df4&oe=5A104D1C
 Mara nyingi huwa ni bacteria aina za Gram-negative ama anaerobic bacteria (wasiotegemea uwepo wa oxygen kuishi), ambao ni wagumu kutibika. Hivyo inachukua muda mrefu sana kwa vidonda kupona. Kanuni hizi ni muhimu kuzingatiwa. 

Walioziweka walifanya tafiti hadi kufikia conclusion hiyo. Tutazisimamia bila kupepesa macho. Kila theatre ijengwe hivi la sivyo tutabomoa.
 Image may contain: 1 person, standing and outdoor
 #HK #HamisiKigwangalla #Dr_Kigwangalla #MzeeWaField #SiasaNiVitendo #ImarishaAfya #StrengtheningHealthSystems #Njombe
 Image may contain: 1 person, standing and outdoor
Andiko la Naibu waziri Afya Dkt Khamisi Kingwangala Kuhusu Ziara yake Mkoani Njombe. Andiko la Naibu waziri Afya Dkt Khamisi Kingwangala Kuhusu Ziara yake Mkoani Njombe. Reviewed by Erasto Paul on July 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.