Mbunge wa
Sengerema, William Ngeleja amesema katika kipindi cha zaidi ya miaka 12
akiwa kiongozi wa umma hakuwahi kukumbwa na kashfa yoyote ya rushwa na ufisadi.
Ameyasema
hayo leo Jumatatu, Julai 10 wakati akitangaza uamuzi wake wa kurudisha Sh 40.4
milioni fedha za mgawo wa Escrow alizozipokea kutoka kwa mfanyabiashara James
Rugemalira.
Amesema
amerudisha fedha hizo kwa kuwa amesononeka na kufadhaika baada ya kuona msaada
aliopewa unahusishwa na tuhuma.
Kuhusu
kuchelewa kurudisha fedha hizo baada ya Rugemalira kutuhumiwa, Ngeleja amesema
alishindwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa haikuthibitishwa kama mfanyabiashara
huyo ana kashfa.
Ngeleja: Fedha za Escrow zimenisononesha na kunifadhaisha
Reviewed by Erasto Paul
on
July 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili