Watu
wasiojulikana wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke,
wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia leo.
Kadhalika
watu hao walimjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu.
Mganga wa
zamu katika Hospitali ya Mchukwi, Dk Emmanuel Humbi amethibitisha kufikishwa
hospitalini hapo kwa mwanamke huyo akiwa na majeraha ya kupigwa risasi na
kusema kwa sasa yupo katika chumba cha matibabu ya dharura.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema tayari polisi wamekwenda
eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.
Ahofiwa kuuawa kwa risasi, mke wake ajeruhiwa
Reviewed by Erasto Paul
on
July 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili