Rais John
Magufuli ameukumbuka mchango wa marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya
Kikwete na kuwashukuru huku akieleza kuwa wao ndiyo waliotengeneza maisha yake
ya kisiasa hadi kuwa kiongozi.
Magufuli
ameyasema hayo leo Jumatatu, Julai 10 wilayani Chato wakati wa uzinduzi wa
nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.
“Nakumbuka
siku hiyo tulikuja hapa Chato na wewe (Mkapa) Msafara ulisimamishwa na
ukawaambia wananchi wa Chato nichagulieni huyu, nakumbuka ulikuwa umevaa viatu
vyekundu,” amesema na kuongeza:
“Kwa
bahati nzuri, wananchi wa Chato wakanichagua, baadaye ukanichagua kuwa naibu
waziri. Wewe ulinitangaza, sikustahili chochote, maneno yako yalikuwa na nguvu
kwa Watanzania.”
Amesema
anamkushukuru pia Rais Mstaafu Jakaya Kkwete na kusema: “Baada ya kipindi cha
Mkapa, Kikwete alipokuja, lakini kwanza wewe ukanipitisha kugombea ubunge tena
kwa mara nyingine, nikachaguliwa bila kupingwa katika jimbo hili.” Amesema
Amesema
hata katika kipindi cha awamu ya nne, Rais Kikwete alimteua katika wizara
mbalimbali.
“Kwangu
mimi nyinyi mlitengeneza maisha yangu katika uongozi. Pia nawashukuru sana
viongozi wa awamu ya kwanza, Nyerere na Mwinyi ambao walitengeneza mazingira
mazuri ndani ya Chama cha Mapinduzi,” amesema na kuongeza:
“Kwangu
mimi sina cha kuwalipa jukumu langu ni kuwatetea na ninawaahidi Watanzania kuwa
nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, namuomba Mungu asinifanye nikawa na kiburi
namuomba asinifanye nikasahau nilipotoka.”
JPM aukumbuka wema wa Mkapa, Kikwete
Reviewed by Erasto Paul
on
July 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili