Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji ya Acacia,
Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa vipindi
viwili.
Mwapachu
amechukua uamuzi huo leo, Julai 13 baada ya muhula wake wa pili wa miaka mitatu
mitatu wa ujumbe wa bodi hiyo, kumalizika.
Taarifa
iliyotumwa leo na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Acacia imeeleza kuwa
inamshukuru Balozi Mwapachu kwa utendaji wake na ushirikiano wake wote
alipokuwa mjumbe.
“Tunamtakia
maisha mema,” imesema taarifa hiyo.
Kutokana
na mabadiliko hayo, Bodi ya Acacia itabaki na wajumbe saba, wakiwamo wanne
wakurugenzi na wasio wakurugenzi.
Mwapachu astaafu ujumbe wa Bodi ya Acacia
Reviewed by Erasto Paul
on
July 13, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili