Ofisi za
Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki kituo cha televisheni cha Star na cha
redio cha Radio Free Africa (RFA) zimefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) kwa deni la Sh4.5 bilioni.
Ofisi hizo
zimefungwa leo Alhamisi (Julai 13) na wakala wa TRA, Kampuni ya Sukah Auction
Mart and Court Brokers ya jijini Mwanza.
Meneja
utumishi na utawala wa Sahara Media Group, Raphael Shilatu amesema ni kweli
wana malimbikizo ya madeni yanayotokana na kuhama kutoka mfumo wa analogia
kwenda digitali.
Deni la kodi Sh4.5 bilioni lasababisha TRA kufunga ofisi za Sahara Media Group
Reviewed by Erasto Paul
on
July 13, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili