Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alijikuta kwenye
wakati mgumu kwa muda wakati akiandamwa na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege
alipokuwa akikipokea kikosi cha Everton.
Waziri
Mwakyembe alikumbana na kadhia hiyo mara baada ya kufika uwanja wa Ndege wa
JNIA saa 2:42 na kuvamiwa na kundi la Wanahabari ambao walitaka atumie cheo
chake kuwaruhusu wafanye kazi zao kwa uhuru.
Awali
waandishi wa habari walizuiwa kuingia Uwanja wa Ndege upande wa VIP ambako
Everton ilikoshukia kwa ajili ya kuchukua matukio, ndipo walipoamua 'kumvaa'
Waziri Mwakyembe ambaye alikuwa katika gari yake na kupaza sauti wakimshinikiza
awatete huku wakiimba kwamba wana imani na waziri huyo.
"Waziri
huyo wa Michezo aliwasikiliza na kuwatuliza kwa kuwambia yeye ndiye mwenye nchi
kwa tukio lile hivyo lazima achukue nafasi yake kwa kuwatetea wanahabari zoezi
ambalo lilichukua zaidi ya dakika 10 ndipo waandishi wakaruhusiwa kuingia
kutekeleza majukumu yao.
"Mtakapoingi
mwisho wenu ni pale kwenye lile ua," alisema Mwakyembe huku akionyesha
umbali ambapo Wanahabari wanapaswa kuishia na kuendelea.
"Mtakaporuhusiwa
na kukiuka masharti ya humu ndani, kuna leo na kesho ikitokea mmezuiliwa wala
sitoingilia kati," alisema Waziri huyo.
Mwakyembe awabeba Wanahabari kuipokea Everton
Reviewed by Erasto Paul
on
July 12, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili