Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka Akiwa na viongozi wa wilaya na mkoa katika kijiji cha Ikovo.
Afisa ardhi wilaya ya Makete mkoani Njombe Bw. Anicas Vilumba amepewa siku Tatu kuanzia Leo ahakikishe Mthamini ardhi aliyefanya uthamini katika kijiji cha Ikovo kata ya Mfumbi wilayani Makete analeta fomu zilizotumika kwa ajili ya shughuli hiyo.
Agizo hilo limetolewa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka katika mkutano wa hadhara alioufanya kijijini hapo wenye lengo LA kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo.
Mgogoro huo unatokana na wananchi kudai mapunjo ya fidia waliyopatiwa
wakati wanahamishwa kutoka kijiji cha Ikovo ya zamani kutokana na eneo
hilo kuchukuliwa na serikali kwa ajili ya hifadhi ya Mpanga Kipengele.
Wananachi wa kijiji cha Ikovo kata ya Mfumbi wilayani makete wakiwa na mkuu wa mkoa wa njombe Christopher Olesendeka katika mkutano wa hadhara.
Mkuu wa mkoa amesema baadhi ya fomu namba moja na namba mbili za uhakiki hazipo hivyo mthamini wa ardhi aliyefanya kazi hiyo anatakiwa kuzikabidhi na azipate ofisini kwake ijumaa ya wiki hii.
Amesema endapo hatapatiwa fomu hizo hadi kufikia ijumaa Mhusika huyo awekwe rumande kwa SAA 48 na baada ya kutoka rumande azipeleke.
Amesema baada ya kupata fomu hizo atafuatilia hatua kwa hatua mwenendo mzima wa suala hilo, kabla ya kuunda tume ya kufanya uchunguzi na baadaye atarudi tena kijijini hapo kwa ajili ya maamuzi, huku akiwatoa hofu wananchi kuwa serikali itahakikisha kila MTU anapata stahiki yake anayostahili na asiyostahili hatapata

Afisa Ardhi Makete-Njombe kukiona cha Mtema kuni.
Reviewed by Erasto Paul
on
July 12, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili