Mbunge wa
Kibamba(Chadema) John Mnyika, ameandika katika ukurasa wake wa twitter akimtaka
Rais John Magufuli ateue Waziri wa Nishati na Madini.
“Mheshimwia
Rais, lini utatuea Waziri wa Nishati na Madini,” ameandika jana Mnyika
Mei
mwaka huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini,
Sospeter Muhongo mara baada ya kupokea ripoti ya kamati ya kwanza
iliyochunguza makontena 277 yenye mchanga wa madini yaliyozuiwa bandarini.
Tangu
wakati huo, hakuna aliyeteuliwa kushika nafasi ya Profesa Muhongo, ingawa Naibu
Waziri Dk Medard Kalemani anaendelea na kazi.
Mnyika ana hamu na Waziri mpya wa Nishati na Madini
Reviewed by Erasto Paul
on
July 13, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili