Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ina
wajibu wa kuboresha mandhari ya bandari na huduma zake ili kuendelea kuwa
msaada kwa nchi nyingine ambazo hutumia bandari hiyo.
Profesa
Mbarawa amesema hayo leo Alhamisi Julai 13 wakati wa hafla ya kusaini mkataba
wa makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Uganda. Mkataba huo unalenga
kuboresha huduma za bandari, usafiri wa maji na reli.
“Tanzania
tunao wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za bandari zilizo bora kwa
wateja wetu ambao ni nchi zinazotuzunguka. Kupitia mkataba huu ubora wa huduma
za usafirishaji wa mizigo utaongezeka sambamba na ukuaji wa biashara,” amesema
Profesa Mbarawa.
Kwa upande
wake Waziri wa Uchukuzi wa Uganda, Bagiire Aggrey ambaye ndiye aliyesaini
mkataba huo kwa niaba ya Serikali yake amesema nchi yake imekuwa ikipendelea
zaidi kutumia bandari ya Dar es Salaam kutokana na gharama zake kuwa ndogo.
“Nchi zetu
zinapaswa kushirikiana katika maendeleo ya nyanja za usafirishaji. Ni lazima
tuiendeleze kwa pamoja kwaaji ya maendeleo ya baadaye,”amesema Aggrey.
Mbarawa asema Serikali ina wajibu wa kuboresha bandari
Reviewed by Erasto Paul
on
July 13, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili