
Serikali imechukua sampuli ya maji ya Mto Msimbazi kwa ajili ya kuyachunguza ili kubaini kiwango cha sumu na ubora wa maji yake kwa matumizi ya binadamu.
Akitoa
matokeo ya awali kwa wanahabari, Meneja wa Maabara ya Mazingira wa
Ofisi ya Mkemia Mkuu, Emanuel Gwae, amesema kipimo cha maji ya Mto Msimbazi,
katika eneo la Jangwani, kinaonyesha maji hayo yana kiwango cha oksijeni
cha milimita3.3.
Amesema
kiwango hicho ni kidogo na kwamba kinachohitajika ni kuanzia milimita
sita.
“Hii
inaonyesha namna ambavyo maji haya yamechafuka na viumbe hai waliomo humu
hawawezi kuishi,” amesema Gwae.
Mchakato
wa upimaji wa maji hayo umefanyika leo, Jumanne, Julai 11 katika tukio ambalo
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga
Mpina alilishuhudia.
Katika
hatua nyingine, Ofisi ya Mkemia Mkuu ilichukua sampuli hiyo ya maji ambapo
Waziri Mpina alishiriki kuchota maji hayo kwa ajili ya kupimwa.
Mbali na
ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wadau wengine waliokuwamo ni pamoja na
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bonde la Wami-Ruvu na Baraza la Usimamizi na
Uhifadhi wa Mazingira (NEMC).
Mpina
amesema kumekuwa na uchafuzi mkubwa katika Jiji la Dar es Salaam unaosababishwa
na baadhi ya viwanda kutokuwa na mfumo wa kutibu maji taka na kusababisha
maji yake kutitirika katika mito.
Amesema
baada ya maji hayo kutiririshwa katika mito, matokeo yake ni kwamba mito
inachafuka na kubadili rangi kutokana uchafu huo.
“Shughuli
za umwagiliaji zinafanyika katika mito hii, sasa kwa kutazama tu haya maji
yanakuwa na mchanganyiko wa kemikali hivi yakichanganywa katika vyakula hali
itakuaje? Ndiyo maana tumeamua kuyachunguza ili kujiridhisha hali ipoje katika
mito yetu,” amesema Mpina.
Mpina
aliwataka wenye viwanda kuacha kutiririsha maji katika mito na kwamba
watakaobainika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya
mwaka 2004.
Kwa mujibu
wa Mpina pamoja na Mto Msimbazi, mito mingine minne iliyoathiriwa ni pamoja na
Mlalakuwa, Ngo’mbe, Kijitonyama na Kibangu.
Mbali na
sampuli hiyo, Mpina aliongoza mchakato wa kuyapima maji katika eneo la Jangwani
ili kubaini kiwango cha oksijeni kilichomo kama ni sahihi kwa viumbe hai
waliomo katika maji hayo kuishi.
wataalamu kutoka katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali hawapo pichani, katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Evelyn Mkoko
Maji ya Mto Msimbazi hatari kwa viumbe hai
Reviewed by Erasto Paul
on
July 11, 2017
Rating:

No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili