
Kutokana na shule ya Msingi Ng'onde kata ya Mlondwe wilayani Makete Mkoani Njombe kukosa Mwalimu wa kike, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete ameagizwa kupeleka haraka Mwalimu wa kike shule ni hapo.
Akizungumza na wananchi shuleni hapo hii Leo baada ya kuzindua vyumba viwili vya madarasa, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ameshangazwa na shule hiyo kuwa na Mwalimu wanne wa kiume wote ilihali shule hiyo ni ya mchanganyiko wa wavulana na wasichana.
Amesema halmashauri iwapeleke Mara moja walimu au Mwalimu wa kile ili irahisishe mawasiliano kwa wanafunzi wa jinsia zote.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa amewaonya wananchi wa kijiji hicho kuacha kujihusisha na kilimo cha bangi na badala yake wajikite na shughuli za maendeleo ikiwemo ukarabati wa vyumba vya madarasa shuleni hapo na kwa kuanza ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji.
Amesema hatua za kisheria hazitaacha kuchukuliwa kwa wale wote watakaokmatwa wakijihusisha na kilimo cha bangi sheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mkuu wa mkoa wa Njombe yupo wilayani Makete akiendelea na ziara ya kikazi ya kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbali mbali ya maendeleo wilayani humo.

SHULE HAINA MWALIMU WA KIKE MAKETE-NJOMBE.
Reviewed by Erasto Paul
on
July 12, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili