Daraja Mto Lukuledi kuwaepusha wananchi kuliwa na mamba




 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtv-hXvbjPIkP4shWPEgwTeEZi7TUlIf1xIeGBCWnO_TFFT0E6kbAr9RQxAyKt3F5htiZGAAu34ZEaLtI83CjoLNdwM2OyJPLODkjy2lTNt8OMb5NuX-2Q9LPbRYl_ZjTC7qZPSW9xLvz6/s1600/PMO_0678.JPG
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa daraja la Mto Lukuledi lenye urefu wa mita 30.45 linalounganisha mikoa ya Lindi na Mtwara.

Amesema ujenzi wa daraja hilo utakaogharimu Sh5.4 bilioni hadi kukamilika ni mkombozi kwa wananchi wa mikoa hiyo na hasa wa wilaya za Ruangwa na Masasi.
Wananchi hao wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kilimo na huduma za kijamii.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo leo Julai 11, alipotembelea mradi huo katika Kijiji cha Nandanga alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi.
“Watu wengi wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba walipokuwa wakikatiza eneo hili. Ujenzi wa daraja hili ni muhimu, watu wengi wa Ruangwa wanavuka kufuata matibabu katika Hospitali ya Ndanda wilayani Masasi na wakazi wa Ndanda wanavuka kufanya shughuli za kilimo wilayani Ruangwa,” amesema.
Waziri Mkuu katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa mkandarasi anayejenga daraja hilo ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kumaliza kazi kwa wakati.
Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe amepongeza jitihada za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo na kubadilisha maisha yao.
Amesema mradi huo ni faraja kwa wananchi kwa kuwa eneo hilo ni makazi ya mamba, hivyo kukamilika kwa ujenzi kutaokoa maisha ya watu na kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa.
Daraja Mto Lukuledi kuwaepusha wananchi kuliwa na mamba Daraja Mto Lukuledi kuwaepusha wananchi kuliwa na mamba Reviewed by Erasto Paul on July 11, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.