Rais John
Magufuli amesema anapenda taasisi zinazohimiza maendeleo badala ya zile
zinazohamasisha wanafunzi wazae kisha warudi shule.
Ameyasema
hayo leo Jumatatu, Julai 10, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 za wahudumu wa
afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation. Hafla hiyo imefanyika katika
Uwanja wa Manzana, Chato.
“Nazipenda
taasisi zinazohimiza maendeleo si zinazotaka watu wazae halafu warudi shuleni.
Mmekalia kusema kuwa watu wazae halafu warudi shule, sasa si watazaa kila
mahali, darasa lote litakuwa na mimba,” amesema.
Amezitaka
taasisi nyingine ziige mfano wa taasisi ya Mzee Mkapa, na kusema ni vyema
kusimama majukwaani na kutangaza vitu vyenye maendeleo.
“Vipo vitu
‘tangible’, taasisi zipo kwenye majukwaa, wanaletewa hela nyingi, lakini
‘impact’ hakuna nani aliyewaambia kuwa kila anayepata mimba amebakwa?” Amehoji
na kuongeza:
“Hata
kwangu kuna watu wanaozaa na wala hawajabakwa, hata mtoto wa mdogo wangu alizaa
bila kubakwa, alipoulizwa imekuwaje (anaongea kwa lugha ya kisukuma) akanizalia
mtoto akamuita John, akakaa kidogo akazaa tena mtoto akamwita Samia.” Amesema
na kusababisha kicheko kwa umati huo.
JPM: Hata kwangu wapo waliozaa wakiwa shuleni
Reviewed by Erasto Paul
on
July 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili