Kagera.
Rais John Magufuli ameagiza Sh200 milioni zilizopangwa kutumika katika
mradi wa maji katika kambi ya jeshi zianze kuimarisha miradi ya maji kwa
wananchi kwanza.
Akizungumza
leo, Alhamisi Julai 20 katika ziara yake akiwa ameambatana na Rais
wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, Magufuli amesema amebaini kuwa pampu za
maji wilayani Ngara zimeharibika kwa zaidi ya wiki tatu na kuwa wilaya hiyo ina
uhaba mkubwa wa maji.
Alimuita,
Mhandisi wa Maji ajieleze ni kwa nini pampu hizo hazifanyi kazi na baada ya
kumsikiliza ndipo alipofanya uamuzi huo.
Akifafanua
kuhusu hali ya maji, mhandisi huyo amesema awali visima vya maji wilayani hapo
vilikuwa vikihudumia watu 400 lakini kwa sasa wilaya hiyo ina watu zaidi ya
240,000 na hivyo visima hivyo havitoshelezi.
“Tulikuwa
tuna idadi ndogo ya watu sasa hivi imeongezeka, lakini tangu pampu iharibike,
tumetengeneza mbili na kisima kimoja hakina pampu,” amesema.
Baada
ya mhandisi huyo kufafanua hayo ndipo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri
kueleza mipango yake, ndipo Mkurugenzi huyo aliposema mradi wa maji wa Sh200
milioni utaanza kwanza katika kambi ya jeshi.
Kauli hiyo
ndiyo iliyomfanya Rais Magufuli kushauri fedha hizo zitumike katika miradi ya
maji katika makazi ya wananchi kwanza.
“Wanajeshi
wapo 200 na wananchi wapo zaidi ya 20,000 sasa si bora waanze wananchi kwanza,”
amesema.
JPM aagiza Sh200 milioni za mradi wa maji jeshini zitumike kwa wananchi
Reviewed by Erasto Paul
on
July 20, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili