Kagera.
Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu
Nchemba kusimamisha kuwapa uraia raia wa Burundi kuanzia sasa.
Akizungumza
leo, Alhamisi Julai 20 wakati wa ziara yake mkoani Kagera, akiwa
ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alimtaka asiwape uraia
wanaotoka nchi nyingine.
“Rais
amezungumza hapa kwa upole, Rais mwenyewe ana hofu ya Mungu, wazazi wake
waliuawa, lakini anataka kushirikiana na Warundi wote kwa nini mnataka kuondoka
kwenu,” amesema.
Awali,
Rais Nkurunziza amezungumza na wananchi hao na kuwataka raia wa Burundi warudi
nchini mwao kwani kwa sasa amani imerejea.
Kadhalika,
Waziri Nchemba amesema katika kipindi cha 2016/17, Tanzania imewapa uraia
wakimbizi wa Burundi 1060.
Pia,
Waziri Nchemba amesema kati ya wakimbizi 247,000 waliopo nchini, 5,000 wameomba
kurudi kwao.
JPM amuagiza Nchemba kusitisha kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi
Reviewed by Erasto Paul
on
July 20, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili