Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe na Mbunge wa Jimbo la Makambako Mh Deo
Sanga a.k.a Jah People akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John
Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Mwandishi; Erasto Paul
Halmashauri
kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa
Njombe Imetoa tamko la kumpongeza Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa utendaji
kazi wake unaosifiwa na wengi.
Tamko
hiyo limetolewa na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM MKOA WA Njombe waliokutana
hii leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Njombe Uliopo Mtaa wa Mji Mwema Chini ya
Mwenyekiti wa Ccm Mkoa Ndugu Deo Sanga amabaye ni Mbunge wa Jimbo la Makambako.
Akisomo
Tamko hilo Mh Deo Sanga amesema Kwa Kauli moja wajumbe Wameazimia Kumpongeza Raisi Kwani
Tangu achaguliweRaisi amejidhihirisha pasipo shaka yoyote kuwa ni kiongozi
Shupavu asiye na uoga wala kuteteleka katika kutete maslahi ya Taifa.
Mh
Deo Sanga amesema Raisi ameonyesha Uzalendo wa kweli katika kulipigania taifa
dhidi ya watu wenye tabia ya kuhujumu Uchumi.
Katika
hatua Nyingine Mh Sanga ametolea mfano
wa mambo ambayo kama mkoa unayatambua na kuyathamini ambayo yamefanywa na Raisi
Kuwa ni pamoja na kupambana na vitendo viovu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi
ya watumishi wa serikali wasio waadilifu.
Amesema
Vitendo hivyo vimekuwa vikipoteza Mapato ya serikali kama vile kulipa mishahara
hewa kwa watumishi,tabia ya uzembe na ubadhilifu wa mali za umma,ukwepaji kodi
na mengineyo.
Aidha
Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Njombe
imesema baada ya kutafakari kazi Nzuri iliytofanywa na Raisi imeridhia
kuwa mwenendo huo utaiwezesha kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda kufikiwa kama
ilivyotarajiwa na ilani ya cahama hicho
kufikia 2020.
Pamoja
na kumpongeza Raisi Hamashauri kuu imetoa wito kwa watanzania kumuunga mkono
kwa kushiriki kwa vitendo kuyapiga vita
maovu katika jamii.
Mkutano huo umehudhuliwa na wajumbe wa halmashauri ya Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe wakiwemo wakuu wa wilaya.
HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA NJOMBE YATOA TAMKO LA KUMPONGEZA JPM
Reviewed by Erasto Paul
on
July 25, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili