Komamanga ni tunda lenye asili ya India
na kisayansi linaitwa Punica Granatum, lakini lililetwa Marekani na wawekezaji wa
Kihispania na kwa sasa limejulikana dunia nzima.
Wataalamu wanasema, Komamanga ni zaidi ya tunda kwa
sababu limejaa vitamini, madini na virutubisho vingi vinavyoweza kuufanya
mwili kuwa na afya na nguvu.
Mbali na hilo, komamanga pia lina vitamin C, B5, A,
E pamoja na madini ya potassium na chuma na unapotumia juisi ya
tunda hilo, husaidia kuponya saratani, na husaidia mtiririko wa damu kwenda
vizuri katika mishipa ya damu, hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo,
shinikizo la damu na kiharusi.
Ulaji wa mara kwa mara wa tunda hili huzuia meno
kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu, bakteria,
maambukizi ya virusi ndani ya mwili, kutibu maradhi ya tumbo ikiwamo kutopata
choo.
Husaidia kuondoa sumu mwilini, hupambana na
tatizo la uzito, husaidia kuua virusi vya aina mbalimbali, lakini kizuri zaidi,
komamanga pia ni mahiri katika kutibu magonjwa ya kusendeka
(magonjwa ya muda mrefu), kama saratani ya tezi dume,
saratani mbalimbali, kisukari, baridi yabisi na uvimbe katika
maungo (gout).
Uchunguzi uliochapishwa katika jarida la Utafiti la
Kuzuia Kansa, umeonyesha kwamba kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza
kuzuia kimeng’enyo (enzyme) aina ya aromatase, hali ambayo huzuia kukua
kwa homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti.
Kiongozi aliyeongoza katika uchunguzi huo, Shiuan
Chen amesema kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen na kusaidia
kuzuia seli za kansa ya matiti kuzaliana mwilini pamoja na tezi la
ugonjwa huo kukua.
Aromatase ni kimeng’enyo ambacho hugeuza homoni ya
androgen kuwa estrogen na kushambuliwa kimeng’enyo hicho ndio lengo kuu
la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen.
(Hadija Jumanne)Mwananachi
DAWA LISHE: Fahamu asili ya komamanga na matumizi yake
Reviewed by Erasto Paul
on
July 07, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili