Wakati
hali ya wasiwasi ikizidi kushamiri kwa wakazi wa wilaya za Kibiti na Rufiji juu
ya usalama wa maisha yao kutokana na kuendelea kwa matukio ya mauaji, hofu hiyo
bado imetanda miongoni mwa wanachama wa CCM wanaohofia kuchukua fomu za kuwania
uongozi ngazi ya matawi na shina.
Akizungumza
na gazeti hili kwa njia ya simu, Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho
katika wilaya hizo, Mussa Mnyeresa amesema sababu za wanachama kususa kuchukua
fomu hizo hasa ngazi za tawi, shina na nafasi nyingine ni mfululizo wa
matukio ya mauaji yanayoendelea katika wilaya hizi.
Amesema
katika wilaya ya Kibiti, kata za Mjawa, Ruaruke na Mchukwi yanaongoza kwa
wanachama wa chama hicho kutochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi.
Aidha
amesema katika wilaya ya Rufiji uchukuaji fomu za nafasi za uongozi Tarafa ya
Ikwiriri yenye Kata tatu za Umwe, Mgomba na Ikwiriri napo zoezi la uchukuaji
fomu wa nafasi hizo si la kuridhisha.
Mnyeresa
amesema hadi sasa kasi ya uchukuaji fomu hizo katika kata hizo bado ipo chini
huku viongozi wa chama hicho wakiendelea kuwahamasisha wanachama wa chama hicho
wachukue fomu.
Amesema
uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya hizo ambazo awali ilikuwa ni wilaya moja
tayari umepeleka taarifa za wanachama kwenye baadhi ya maeneo kutochukua fomu
za kugombea nafasi mbalimbali wakihofia usalama wao.
Akizungumza
juu ya wanachama kuchukua fomu za uongozi Ngazi ya Tawi na Shina katika wilaya
ya Kibiti, Katibu wa chama hicho wilayani hapa, Zena Mgaya amesema hali ya
uchukuaji fomu kwenye ngazi hizo hairidhishi.
Zena
alisema katika ngazi za uongozi za kata na wilaya hali inaridhisha na wanachama
wamehamasika kuchukua fomu hizo.
Amesema
hadi sasa kati ya kata 16 zinazounda wilaya ya Kibiti, tayari wamepokea fomu za
kata 10 za wagombea wa nafasi za tawi na shina.
Amesema
kwa upande wa nafasi za uongozi wa ngazi za kata na wilaya, bado wanachama
wanaendelea kuchukua fomu na kuzijaza.
Zena
amesema pamoja na kuwepo hofu ya mauaji kwa wananchi na wanachama wa chama
hicho, bado mwitikio ni mzuri zaidi kwenye nafasi za kata na wilaya.
Akizungumzia
wanachama wa chama hicho kutochukua fomu hasa za ngazi ya tawi, mmoja wa
wanachama wa chama hicho, ambaye pia ni Diwani Kata ya Mtawanya, Malela Tokha
amesema ni vyema uongozi wa chama hicho ngazi ya taifa ukayafanyia kazi maombi
ya wanachama wa chama hicho waliyoomba uchaguzi huo usogezwe mbele.
Amesema
hali hiyo itaepusha chama hicho kupata viongozi wasiokuwa na sifa na uwezo na
kuzidi kukidhoofisha chama kwa kuwa wakati huu wanachama wenye uwezo wengi wao
wanaogopa kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi.
CCM washindwa kuchukua fomu Kibiti
Reviewed by Erasto Paul
on
July 14, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili