Rais wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli ameteua wajumbe wa kamati maalum ya pili itakayofanya
uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya
makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
makontena yenye mchanga wa madini yaliyozuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam
Kamati
hiyo inajumuisha wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamati ya
kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na
uchambuzi wa kisayansi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni;
Prof. Nehemiah Eliachim Osoro Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara Dkt. Oswald Joseph Mashindano Bw. Gabriel Pascal Malata Bw. Casmir Sumba Kyuki Bi. Butamo Kasuka Philip Bw. Usaje Benard Usubisye Bw. Andrew Wilson Massawe
Wajumbe hao wataapishwa na Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 11 Aprili, 2017 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Hii ni kamati ya pili ya kulifuatilia
suala hilo, baada ya Rais kuunda kamati nyingine wiki iliyopita, ambayo
imesheni wataalam wa masuala ya madini na miamba.
Kamati nyingine yaundwa kuchunguza mchanga
Reviewed by Erasto Paul
on
April 10, 2017
Rating: 5
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili