Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesikitishwa na vitendo
walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki na wenzake huku akisema
hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa yanaendelea kutokea.
Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akizungumza na wanahabari
Akizungumza
na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema
kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi
kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu
sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya
wizara yake.
"Hiki kilichotokea siyo hali
ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali kitu kama hiki kiendelee
kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana, nitajitahidi nipate majibu
kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema Dk. Mwakyembe
Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka
wananchi waache tabia ya kuamini kila maneno yanayosemwa na watu ambao
hawana ujuzi katika masuala ya uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda
vyombo vya dola viweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.
"Nilishasema kuwa nimeagiza
vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili ajulikane aliyewafanyia hivi
wakina Roma kama ni nani kama wa dola ntadili naye, tuache uchunguzi
ufanyike, tuache kupiga ramli". Alisisitiza Mwakyembe
Roma Mkatoliki
Pia Waziri huyo mwenye dhamana na
wasanii ametoa ujumbe kwa vyombe vyote vilivyopo chini ya Wizara yake
kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo
taarifa kamili kutoka kwake.
Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye
amesimulia tukio lilivyokuwa amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi
kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna
mambo akiyaweka hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.
Pia amesema hawezi kujua kama
kweli tukio hilo lililowatokea linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza
kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani ambaye hana hata chembechembe
za uimbaji.
Mwakyembe aapa 'kufa' na waliomteka Roma
Reviewed by Erasto Paul
on
April 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili