Serikali imesema watu 6,529
wamefariki dunia huku watu 30,661 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajali
31,928 zilizosababishwa na pikipiki maarufu bodaboda na bajaji katika
kipindi cha miaka saba kati ya Januari 2010 hadi Februari 2017.
Moja ya matukio ya ajali zinazohusisha bodaboda
Akijibu
swali la mbunge Abdallah Haji Ali wa jimbo la Kiwani, aliyeuliza ni
watu wangapi wamepoteza maisha na wangapi wamejeruhiwa kwa ajali za
bodaboda kuanzia mwaka 2010 hadi 2017.
Waziri wa mambo ya ndani, mheshimiwa
Mwigulu Nchemba, amesema usafiri wa bodaboda na bajaji ulianza mwaka
2008, lakini serikali ilipitisha kanuni na masharti ya usafirishaji
mwaka 2010, lakini hakuwa na utaratibu wa kusimamia biashara hiyo.
Mheshimiwa Nchemba amesema kipindi cha
Januari 2010 hadi Februari 2017, kumekuwa na jumla ya ajali 31,928
zilizosababisha vifo vya watu 6,529 na majeruhi 30,661.
Bodaboda zaua watu zaidi ya 6,000
Reviewed by Erasto Paul
on
April 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili