Mbunge wa jimbo la Nzega
Mjini kupitia tiketi ya CCM, Hussein Mohamed Bashe amesema ametumiwa
ujumbe wa vitisho kuwa yeye ni miongoni mwa watu 11 waliopo hatarini
kufanyiwa vitu vibaya popote pale watakapoonekana ikiwemo kuundiwa
ajali.
Hussein Bashe Bungeni
Bashe
amebainisha hayo leo wakati akiomba muongozo Bungeni ambapo alitaka
Bunge liahirishe shughuli zake ili kujadili matukio hayo ya utekaji
ikiwa ni pamoja na vitisho hivyo na kubainisha kuwa kuna wabunge wengine
akiwemo Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Musukuma, ambao wamo kwenye
orodha ya watu wanaowindwa.
Katika maelezo yake Bashe amesisitiza
kuwa Bunge na Serikali haviwezi kulifumbia macho jambo hilo haramu
ambalo kwa sasa imekuwa gumzo katika midomo ya watu masuala ya utekaji
watu na kuwapeleka kusipojulikana.
"Kuna watu wamenitumia
ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu
vibaya popote pale tulipo. Bunge na Serikali haviwezi kulifumbia macho
jambo hili la haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana". Ameandika Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa twitter
Aidha Bashe amesema kuwa kikundi
kinachohusika na matukio ya utekaji kiko ndani ya Idara ya Usalama wa
Taifa na kwamba hao ndiyo waliohusika na tukio la kumteka msanii Roma
Mkatoliki.
Roma Mkatoliki
Kwa upande mwingine Mbunge wa Kigoma
mjini, Zitto Kabwe amempa pole mwenzake na kumtaka amtumainie Mungu kwa
kuwa ndiye anayejua mwisho wetu.
"Allah ndiye anajua mwisho wetu wote. Hao wanaotuwinda watajikuta ndiyo wanawindwa na mola. Tusiogope. Tupambane". Ameandika Zitto
Wakati huo huo, Mbunge wa Mbeya Mjini
Joseph Mbilinyi 'Sugu' pia aliomba muongozo kwa spika kukazia hoja ya
Bashe akitaka Bunge liahirishwe, huku akimtaka pia Waziri wa Mambo ya
Ndani Mh. Mwigulu Nchemba kuachia ngazi kwa kuwa ameshindwa
kuwahakikishia wananchi usalama wao.
Hata hivyo Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
akijibu muongozo huo, alisema kwa mujibu wa kanuni, jambo hilo
halijakidhi vigezo vya kufanya shughuli za Bunge liahirishwe
Bashe naye atishiwa kupotezwa
Reviewed by Erasto Paul
on
April 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili