Serikali imesema kuwa hakuna
mwekezaji yeyote aliyeruhusiwa kupewa kibali cha kuingiza vifaranga au
mayai ya kuku nchini kwa ajili ya biashara.
Katika kusimamia hili, kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67,500 vilivyoingizwa nchini kinyume na sheria viliteketezwa.
Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Naibu
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvivu, Mhe.William Ole Nasha amesema
wapo wawekezaji wachache ambao hupewa vibali maalum vya kuingiza mayai
au vifaranga wa kuku wazazi (Parent Stock) pekee na ukaguzi kwa ajili ya
kudhibiti uingizaji vifaranga na mayai unaendelea.
Amesema hatua kali zinachukuliwa kwa yeyote anayekamatwa kwa kukiuka utaratibu.
Marufuku mayai na vifaranga kutoka nje
Reviewed by Erasto Paul
on
April 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili