ENDELEA ILIPOISHIA: Uombaji
radhi ulifanyika katika shughuli maalum iliyoandaliwa na viongozi wa
Jimbo la East New Britaish na shughuli hiyo ilipewa jina la
‘reconciliation ceremony’ yaani sherehe ya maridhiano na ilifanyika
Rabaul, mji mkuu wa jimbo hilo ambalo lina wenyeji ambao ni wala watu.
“Katika kipindi hiki tumeguswa na
kitendo kile na tunaomba msamaha na tunaamini leo tunafuta rekodi hii
(ya kuuawa kisha kuliwa kwa mchungaji na wenzake),” alisema Gavana wa
jimbo hilo, Ratu Isoa Tikoca.
Ulaji wa watu ni kitu cha kawaida kwa
watu wa sehemu za South Pacific , kwa mfano, Kisiwa cha Fiji kilikuwa
kikijulikana kama Kisiwa cha Wala Watu na madazani ya wamisionari
waliuawa eneo hilo na kuliwa na wenyeji wa hapo.
Mchungaji Brown alikuwa anajua kwamba
wenyeji wa visiwa vya Papua Newa Guinea ni wala watu. Aliwahi kuandika
katika makabrash yake kwamba katika pitapita yake kisiwani humo
akihubiri aliwahi kutembelea kijiji kimoja akakuta mifupa 35 ya mataya,
viganja vya binadamu ikiwa imebanikwa ikiwa kwenye moja ya vibanda
kijijini hapo.
“Mikono ya binadamu iliyookwa niliikuta
ikiwa inaning’inizwa katika moja vibanda kijijini, nje kulikuwa na mnazi
ambao ulikuwa na alama 76 ambazo wenyeji walituambia kila alama
inawakilisha mtu mmoja aliyepikwa nyama yake na kuliwa hapa,” alisema
Mchungaji Brown enzi za uhai wake alipokuwa akiwaambia viongozi wa
Taasisi ya Royal Geographical Society.
Maneno hayo aliambiwa akiwa hajui kwamba
wamisionari wenzake wa dhehebu la Methodist aliokuwa nao, tayari nao
wameliwa huko alikowatuma kuhubiri na alipojua, aliingiwa na wasiwasi
mkubwa juu ya maisha yake.
“Waliuawa na kuliwa kwa sababu tu,
walikuwa wageni na wenyeji waliofanya hivyo hawakuwa na sababu nyingine
isipokuwa walikuwa na tamaa ya kula nyama zao na kuchukua baadhi ya mali
chache walizokuwa nazo,” aliandika Mchungaji Brown.
Kulitokea vurugu kati ya wenyeji na
Wazungu kutoka Ulaya baada ya kitendo cha kuliwa watu hao weupe kwani
vijiji kadhaa vilichomwa moto na mitumbwi ya wenyeji iliharibiwa.
Makabila kumi ya visiwa hivyo yalilaumiwa kwa kushambulia wazungu na
kuwala nyama hasa katika eneo linaloitwa Blanche Bay. Mchungaji Brown
aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa London Missionary Society aliandika
hivi kabla ya kujua kuwa naye alikuwa
Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep
Tayyip Erdogan akiongea na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli
katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa
BoT jijini Dar es salaam jana Januari 23, 2017 ambapo wamesaini
mikataba 9 ikiwemo ya sekta ya anga, elimu, utafiti n.k.
KARIBU TANZANIA
akiwindwa aliwe: “ Wenyeji
wanatu-heshimu kuliko mwanzo, hii ni kwa sababu wanajua haki tuliyonayo
inayotuumiza mioyo ya kuwaelimisha.” Hata hivyo, kuna taarifa kuwa
Michael Rockefeller (pichani), aliyekuwa mtoto wa Makamu wa Rais wa
Marekani, Nelson Rockefeller mwaka 1961 naye aliuawa na kuliwa nyama
yake na watu hao. Ilikuwaje? Fuatilia Jumanne ijayo uone yaliyompata.
Basi hili linafanya safari kutoka Wilaya ya Kilolo vijijini huko Lulanzi kuja Iringa mjini kila siku na kurudi.
Eeeh Mwenyezi Mungu zilaze Roho za marehem pema peponi na uwajaalie majeruhi wote kupona haraka, Amen.
Kabila la wala watu-3: Kumbe Mtoto wa Makamu wa Rais wa Aliliwa na Watu Hao
Reviewed by Erasto Paul
on
January 24, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili