MWAFRIKA wa kwanza kupata Tuzo
la Nobel ambaye ni raia wa Nigeria anayeishi nchini Marekani, Wole
Soyinka (pichani juu), ametimiza ahadi ya kuichana green card yake kama
alivyoahidi hapo awali iwapo Donald Trump angeshinda urais wa Marekani,
shirika la habari la AFP limeeleza.
Mwezi uliopta, mshindi huyo wa tuzo ya
Nobel ya Fasihi mwaka 1986, alisema kuwa angeichana green card, ambayo
humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Donald Trump
angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Donald Trump.
Soyinka aliyezaliwa Julai 13, 1934
nchini Nigeria na kupata elimu yake Uingereza, aliliambia Shirika la AFP
mjini Johannesburg kuwa kutokana na ushindi wa Trump, basi ametekeleza
alichokisema.
“Tayari nimeishafanya, nimetoka
Marekani, nimefanya kile nilichosema kuwa nitakifanya, nimechana green
card yangu , nimerudi sehemu ninayostahili kuwa,” alisema Soyinka.
Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine wanaoishi Marekani kufuata uamuzi wake huo aliouchukua.
Soyinka Aichana Green Card Yake, Ni Baada ya Kutoa Ahadi Hiyo Iwapo Trump Angeshinda Uchaguzi
Reviewed by Erasto Paul
on
December 02, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili