SHINYANGA: Mganga wa kienyeji
‘Sangoma’ aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55), mkazi wa
kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani Shinyanga ameuawa
kwa kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.
Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) alikwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa
wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio hilo ni la Novemba 29 mwaka huu,
akisema lilitokea majira ya saa tano asubuhi.
Alisema Kashinje alifariki dunia
alipokuwa anakimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha
kali katika jicho la kulia na kupigwa kwa fimbo mgongoni na watu
waliojichukulia sheria mkononi.
“Watu hao walijichukulia sheria
mkononi baada ya mganga huyo kujaribu kumbaka mwanamke (jina
linahifadhiwa), mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga
ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze kupata mtoto”, alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda Muliro alibainisha kuwa chanzo
cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na uongo wa kimatibabu wa kutaka
kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya kumlewesha kwa dawa za
kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga kelele na ndipo wananchi
walipomvamia mganga huyo.
GPL
Sangoma Auawa Akitaka Kumbaka Mgonjwa
Reviewed by Erasto Paul
on
December 01, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili