WATU wanaodaiwa kuwa majambazi
wamevamia mgahawa wa Dinners uliopo katika mtaa wa Kenyatta Road jijini
Mwanza na kupora kiasi cha fedha kisichojulikana na kujeruhi watu wawili
kwa risasi kabla ya kutoweka.
Tukio hio limetokea katika eneo ambalo
limezungukwa na taasisi za kibenki ikiwemo benki ya NMB, Kenya
Commercial Bank KCB na wakala wa benki ya CRDB na zote zikilindwa na
askari ambao hawakuweza kutoa msaada wowote licha ya kuwa ndani ya mita
30 kutoka katika mgahawa huo.
Moja ya watu waliojeruhiwa alikuwa ni
muuza mitumba nje ya mgahawa huo na mwingine akiwa na asili ya Asia
ambaye haijajulikana alikuwa nani katika mgahawa huo.
Akizungumza katika tukio hilo, Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amekiri kuwepo kwa tukio hilo na
kusema atazungumza na vyombo vya habari kesho (leo) baada ya kupata
taarifa kamili.
Source;GPL
Majambazi Wavamia Mgahawa, Wapora na Kujeruhi Mwanza
Reviewed by Erasto Paul
on
December 01, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili