Wanasayansi
wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani
Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.
Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth
nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na
mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani. Mmoja wa wanasayansi hao
alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi
majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya
Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81. Wanasayansi nchini
Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo. Wanasayansi
waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti
isiyo ya kawaida duniani.
GPL
Mti Mrefu Zaidi Afrika Wagunduliwa Tanzania
Reviewed by Erasto Paul
on
December 01, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili