Ndege
iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil
ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa
zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia
mawasiliano.
Katika mnara wa mawasiliano ya ndege,
rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa
dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na
kuishiwa mafuta ya ndege.
Kabla hata mawasiliano hayo
yaliyorekodiwa kufikia mwisho, rubani alisikika akisema yuko angani
umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia saba na arobaini na
tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo katika mitandao kadhaa
nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari nchini humo, na hivyo
kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda zikawa na chembe ya ukweli
kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha ajali ya ndege hiyo.
Wanajeshi wa Colombia waliliambia
shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na ndege hiyo kuanguka kuna
shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege hiyo kuanguka hakukuwa na
mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika nguvu ingine tofauti na
nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.
Wadadisi wa mambo na wachunguzi bado
hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia juu ya chanzo chochote cha
ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya uchunguzi itatolewa baada ya
miezi kadhaa.
Wachezaji wa timu ya Chapecoense
walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian kwenye mji wa Medellin
mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa miguu ya kihistoria na
badala yake wachezaji hao wameacha historia .Kufuatia vifo vya wachezaji
wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana kuomboleza vifo vyao.
Kwa muujibu wa taarifa zilizopatikana
kutoka katika shirika la ndege la Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na
ndege hiyo wameponea chupuchupu kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya
kukosa tiketi.
Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye
ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza namna alivyokwepa kifo, kwamba
yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya kujiokoa ,anasema abiria wenzie
, walio wengi walisimama na kuanza kupiga kelele nay eye aliamua kuweka
sanduku lake la kusafiria kati kati ya miguu yake na kuamua kubaki
hivyo.
Visanduku viwili vya mawasiliano vya
ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari vimeanza kufanyiwa uchunguzi na
wataalamu wa masuala ya anga.
Wachunguzi wataalamu kutoka nchini
Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika Kusini kwasababu ndege
iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa Uingereza BAE nchini
Uingereza.Brazil imeanza siku tatu za maombolezo wakati maelfu ya watu
na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika mji yaliko makao makuu
ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa maombolezo wakati maandalizi
ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil
ili kuzikwa kwa pamoja katika uwanja wa Chapeco.
Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.
Timu hiyo iliandika historia ya
mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi ya Brazil kwamara ya
kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa wameabiri ndege hiyo
miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika .Abiria walio wengi
walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na waandishi habari wapatao
ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza maisha.
Sababu za Kuanguka kwa Ndege ya Brazil Zatajwa, Mnusurika Aaanika Mazito!
Reviewed by Erasto Paul
on
December 01, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili