“Wakati niligundua kuwa nilikuwa na
virusi vya HIV, nilijua kuwa nilikuwa na jukumu la kueneza habari kuhusu
njia HIV unaweza kuambukizwa, unaweza kuzuiwa na pia njia za kumaliza
unyanyapaa,” Kasume alisema.
Katika sehemu kubwa ya maisha yake,
amethirika na virusi vya HIV. Alilelewa kijijini na aliwapoteza wazazi
wake wote kwa ugonjwa wa ukimwi akiwa na umri wa miaka 14 na kisha
akaolewa akiwa na umri wa miaka 18.
Akiwa na ndoto na kuona kizazi kichajo
kisicho na virusi vya ukimwi, uamuzi wake wa kutangaza hadharani hali
yake ulizua tofauti kubwa.
Kanisa lake lilimtimua kwa kuchukua
hatua hiyo na kwa kwenda kinyume na matakwa ya mmewe kuhusu kuweka siri
hali yake ya kuishi na virusi vya ukimwi.
Amesafiri sehemu mbali mbali za dunia na
kukutana na viongozi wakiwemo marais wa zamani nchini Marekani wakiwemo
Bill Clinton na George W Bush pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki-moon. Wakati mmoja akitoa hotuba, aliwakumbusha wabunge wenzake
kuhusu umuhimu wa kupimwa hali zao.
GPL
Mbunge Afukuzwa Kanisani kwa Kusema ana Virusi vya HIV
Reviewed by Erasto Paul
on
December 01, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili