Baada ya kuona tukio hili la Amerika
Kusini kutokea ajali ya ndege ambapo wachezaji wamefariki katika tukio
hilo la simanzi lakini sio la kwanza kutokea yapo matukio mengi makubwa
ambayo kupitia Mtembezi.com tunakupatia manne makubwa kati ya yote
yalitokea ili ukumbuke , wakati mwingine matukio kama haya
yanatukumbusha uwepo wa Mungu hivyo tureje kwake kwa mema.
1.1993
Mwaka huo ulikuwa mwaka wa aina yake na
mwaka ambao kwa Bara la Afrika ulikuwa wa majonzi sana haswa baada ya
kutokea ajali ya Ndege ya jirani zetu Zambia ambapo walikuwa wanaelekea
Senegal kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia wakitumia ndege ya
kijeshi. Msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 18 na ‘staff’ 12
walipoteza maisha ila wachezaji 2 ambao walikuwa wanacheza nje walipanga
kusafiri na usafiri mwingine ndio waliopona. Na mmoja ya waliye
nusurika alikuwa Kalusha Bwalya ambapo ndio Rais wa shirikisho la soka
Zambia.
2.1958
Februari 6, 1958, Uingereza ilikuwa katika majonzi ilifanya jaribio lake la tatu baada ya kufunikwa wakitokea Munich-Riem Uwanja wa Ndege wa Munich, Ujerumani Magharibi. Ndege ilikuwa ya timu yasoka ya Manchester United pamoja na idadi ya wafuasi na waandishi wa habari. 23 na watu 44.
3.1987
Mwaka mwingine huo ambao unahistoria
mbaya kwa nchi ya Peru baada ya kupata ajali ya Ndege baada ya ndege
aina ya Navy Fokker F27-400M kuingia katika bahari ya Pacific kama maili
6 na kupoteza wote waliokuwemo ndani yake ambapo walikuwa watu 44.
4.1980
Kwa upande wa masumbwi sasa nao walipata ajali ikiwa machi 14 mwaka 1980 tukio hilo lilisababishwa na ndege kushindwa kwa mitambo ya ndege hiyo na watu zaidi ya 87 kupoteza maisha katika tukio hilo.
MATUKIO MANNE YA KUHUDHUNISHA AJALI YA NDEGE
Reviewed by Erasto Paul
on
November 30, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili