Dhamana ya Lema Bado Ngoma Nzito na Leo Imekwama Tena,


 http://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2016/12/IMG-20161220-WA0033.jpg
Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa 
 yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016 

Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maamuzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa mshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 desemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017

Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?

Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja 

Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama. 
Dhamana ya Lema Bado Ngoma Nzito na Leo Imekwama Tena, Dhamana ya Lema Bado Ngoma Nzito na Leo Imekwama Tena, Reviewed by Erasto Paul on December 28, 2016 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.